Thursday, December 10, 2015

UPUUZI WA CCM HUU  HAPA

Hawa CCM Sasa Wanazeeka vibaya, Yaani Utoe Mbunge Zanziba Aje Apige Kura Za Kuchagua Meya Kinondoni? Huo Ni Upuuzi Mwingine Unaofanywa Na CCM

Tuesday, March 18, 2014

VIPAJI VIPYA 36 VYATAJWA KUOKOA TAIFA STARS


Jopo wa wang’amuzi vipaji limetangaza majina ya wachezaji 36 waliopataikana katika mchakato wa maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha mechi za mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema jopo hilo liling’amua vipaji 143 katika mchakato, lakini waliochukuliwa kwa sasa ni hao 36 tu.
Amewataja wachezaji waliochaguliwa katika mchakato huo kwa upande wa makipa ni Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi), Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga), Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri Ali (Kaskazini Unguja).
Kwa upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba (Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).
Mabeki wa kati ni Abbas Ali Haji (Kaskazini Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma Namwamba (Temeke), Hussein Juma Akilimali (Njombe), Joram Nasson (Iringa), Kayombo Silvanus Henrico (Ilala), Miraji Maka (Mwanza),  Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini Unguja) na Said Juma Ali (Mjini Magharibi).
Viungo wapo Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga), Juma Said Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga), Ryna Mgonyike (Temeke) na Yusuf Mpilipili (Temeke).
Washambuliaji ni Abdallah Kagumbwa (Temeke), Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Athanas Fabian Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu (Mwanza), Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Chunga Said (Manyara), Mbwana Mshindo Mussa (Tanga), Michael David Mlekwa (Lindi), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar Athuman Nyenje (Mtwara), Paul Michael Bundala (Ilala), Ramadhan Kapalamoto (Kinondoni) na Roman Nyapunda (Temeke).
Amesema wastani wa umri wa wachezaji hao ambao watafanyiwa vipimo vya afya Machi 19 na 20 mwaka huu kabla ya kambini Machi 21 mwaka huu, Tukuyu mkoani Mbeya ni miaka 21.
Timu hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na makocha Hafidh Badru, Salum Mayanga na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu utafanyika mchujo ili kupata wachezaji wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa Stars watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.

HATIMAYE ANDER VILLAS-BOAS KOCHA MPYA ZENIT
Zenit St Petersburg wamethibitisha uteuzi wa Andre Villas-Boas kama mbadala wa kocha Luciano Spalletti.

Kocha wa kiitaliano Spalletti alitimuliwa na klabu hiyo ya Russia wiki iliyopita baada ya kukaa kwenye timu hiyo kwa miaka mitano kufuatia mwenendo mbaya wa timu katika ligi na ulaya, baada ya kuchapwa 4-2 na Borrusia Dortmund katika mchezo wa kwanza raundi ya 16 bora.

Na Villas-Boas, ambaye amekuwa hana kazi tangu alipofukuzwa na Tottenham mwezi December mwaka jana amechukua nafasi yake kwa kusaini miaka miwili.

"Zenit wamefikia makubaliano ya mkataba wa miaka miwili na kocha Andre Villas-Boas," taarifa ya klabu ilisema.

"Mkataba utasainiwa na Villas-Boas atatambulishwa mjini St Petersburg kuwa kocha mkuu mpya wa Zenit March 20. Mkataba wa Villas-Boas unaanza March 2014 na utaendelea kwa miaka miwili." 


Kocha huyo amewahi kufundisha klabu ya fc porto ya nchini ureno, chelsea na Totenham zote za nchini england

Monday, December 24, 2012

Sunday, November 25, 2012

STARS WAANZA MAZOEZI - SAMATTA NA ULIMWENGU BADO HAWAJAFIKA KAMBINI

Kipa wa Kilimanjaro Stars, Juma kaseja akitoka Uwanja baada ya
kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha
Kampala Kampasi ya biashara nchini Uganda jana. Stars inadhaminiwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Edward Christopher
akikokota mpira wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo
Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara nchini Uganda jana kwa kujianda
na mchezo wa michuoano ya Cecafa. Stars inadhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakitoka Uwanjani baada ya kufanya
mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara
nchini Uganda jana. Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium
Lager


Na mwandishi wetu,
Kampala

Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema
ana imani na timu yake itakayotupa karata ya kwanza leo (Jumapili) dhidi ya Sudan katika mashindano ya CECAFA Challenge.

Alisema suala la wachezaji  Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kutofika mpaka sasa halimtatizi kwa kuwa ameiandaa timu vizuri na atawatumia wachezaji waliopo.
 “Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.


Kuhusu wachezaji kama Aggrey Morris, Mohamed Nassoro na Mwadini Ali kutoka Zanzibar kujiunga na wenzao kuichezea Zanzibar Heroes, Poulsen alisema pengo lao halitampa tatizo kwa kuwa ni changamoto.


“Timu hii ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa sasa ina wachezaji wengi chipukizi kwa hivyo huu ndio muda wa kuwapima vizuri kwani kwani  haya ni mashindano makubwa,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza  dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.


Timu za kundi A zilitarajiwa kucheza jana ambazo ni Kenya dhidi ya Uganda na Ethiopia dhidi ya Sudan Kusini.
Kundi C inajumuisha Zanzibar na Eritrea na Rwanda dhidi ya Malawi.

Sunday, November 25, 2012

UGANDA YAWACHINJA KENYA KATIKA UFUNGUZI WA CHALENJI CUP

KOMBE LA CECAFA LINALOSHINDANIWA...WENYEJI Uganda, The Cranes wameanza vema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuilaza Kenya, Harambee Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mandela, uliopo Namboole, Kampala, Uganda.Shukrani kwake, mshambuliaji wa Saigon Xuan Thanh ya Vietnam, Geoffrey Kizito aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 74, akiunganisha krosi ya...Read More